Msimamizi mkuu wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq Sayyid Jawadi Hasanawi, mkuu wa ofisi ya katibu mkuu, rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Ali Azhar wamekakua maandalizi ya shule za Al-Ameed kuelekea mahafali.
Azhar amesema “Tukiwa pamoja na msimamizi mkuu wa mahafali Sayyid Jawadi Hasanawi, tumeangalia maandalizi yaliyofanywa na shule za Al-Ameed ambazo ndio mwenyeji wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu katika mwaka wa masomo 2023, mahafali hii inapewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya pamoja na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi”.
Akaongeza kuwa “Maandalizi yako vizuri katika sekta zote, kazi kubwa imefanywa kuhakikisha mahafali inafanyika vizuri kama ilivyo pangwa”.
Akasisitiza kuwa, vitengo vyote vinavyo husika na mahafali haya vimejipanga vizuri kwa ajili ya kufanikisha mahafali ya wahitimu wa vyuo.