Kwa picha.. wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq wanafanya ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq wamefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ikiwa ni sehemu ya shughuli za mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq awamu ya pili.

Kabla ya kufanya ziara wamesoma kiapo cha kuhitimu chuo mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), alasiri ya Ijumaa wakati wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mahafali ya mwaka huu inafanywa chini ya kauli mbiu isemayo “Kutoka ardhi ya Karbala ukarimu unachanua”, ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel kikosi cha (Juu ya muongozo wa mwezi awamu ya pili), imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq.

Wameimba wimbo wa kuhitimu chuo na kula kiapo cha utii mbele ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), tukio hilo limeongozwa na mjumbe wa kamati kuu ta Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Mussawi.

Walianza kumzuru Imamu Hussein kisha wakaja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) wakipita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Siku ya Ijumaa, mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq imefanywa, imepata washiriki kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kuanzia kaskazini hadi kusini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: