Kumaliza sehemu ya kwanza ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.

Imekamilika sehemu ya kwanza ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq iliyopewa jina la (Juu ya uongozu wa mwezi awamu ya pili).

Awamu ya pili ya mahafali hii mwaka huu inakauli mbiu isemayo “Kutoka katika ardhi ya Karbala ukarimu unachanua”, ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi.

Wanafunzi zaidi ya 3000 kutoka vyuo vikuu tofauti wameshiriki, wamesoma kiapo cha utii mbele ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), tukio hilo limeongozwa na mjumbe wa kamati kuu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi.

Siku ya Ijumaa, mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq imefanywa, imepata washiriki kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kuanzia kaskazini hadi kusini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: