Sayyid Swafi amesema: Nyie ni umma bora unaotumika kujenga taifa.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amewaambia wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq kuwa wao ni umma bora unaotumika kujenga taifa.

Ameyasema hayo katika mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq wa mwaka 2023.

Sayyid Swafi amesema “Leo mpo katika mlango wa kuhitimu vyuo na kuingia katika ujenzi wa taifa, lazima mjiamini na mfahamu mahitaji ya taifa hili, mtambue kuwa hamna upungufu wowote na muda unaenda mbio, simameni imara nyie ndio umma bora mnaotakiwa kujenga taifa”.

Akaongeza kuwa “Mnatakiwa kuomba ushauri kwa mtu muaminifu, mueleze fikra zako yule anayekutakia mema, nyie ndio hazina ya taifa na nguvu kazi imara mnaotakiwa kusaidia jamii katika sekta tofauti”.

Akaendelea kusema kiongozi mkuu wa kisheria “Kuna majukumu mawili yanakusubirini, jukumu la kujenga taifa na familia, jengeni familia zenu katika misingi sahihi chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s), elekezeni familia katika njia ya haki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: