Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imehitimisha semina ya Sayyid Abu Qasim Khui inayohusu (maarifa ya Qur’ani).
Semina hiyo imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.
Msimamizi wa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini awamu ya saba, Shekhe Wasaam Sibti amesema: “Semina inahusisha hatua ya pili kwa wanafunzi wa Dini, baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya semina maalum ya (Hukumu za usomaji)”.
Akaongeza kuwa “Semina iliyofanywa katika Shule ya Shekhe Hilliy imehitimishwa kwa wanafunzi kupewa mtihani wa mwisho”.
Sibti akasema: “Lengo la semina hii ni kutengeneza jamii ya wasomi wa Qur’ani wenye emilimu ya maarifa ya Qur’ani na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kupitia program tofauti zinazofanywa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake yaliyopo kwenye mikoa tofauti”.