Kitengo cha habari na utamaduni kimetangaza kufanyia maboresho toghuti yake.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza kufanya maboresho katika toghuti yake, maboresho hayo yanahusisha kubadilisha muonekano wa nje na namna ya kuangalia vipengele vyake.

Rais wa kitengo Sayyid Aqiil Yasiri amesema “Toghuti rasmi ya sasa inatofautiana na yazamani, imeongezwa vipengele vya elimu, utamaduni, harakati, habari, makongamano, nadwa, majarida, vitabu na nyaraka mbalimbali”.

Akaongeza kuwa “Toghuti mpya inavipengele vingi vinavyo funguka kwa urahisi na vinaendana na maendeleo ya sekta hiyo”.

Akabainisha kuwa “Tumefanya maboresho mapya kwa ajili ya kuonyesha huduma zote zinazotolewa na kituo hiki pamoja na idara zake”.

Rais wa kitengo akaendelea kusema “Kuna kazi kubwa imefanywa kwa ajili ya kufanikisha jambo hili, watumishi wa kitengo cha habari na kituo cha mitandao ya kijamii wanamchango mkubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: