Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Hamza bun Abdulmutwalib (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Hamza bun Abdulmutwalib (a.s).

Majlisi imesimamiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Majlisi imefanywa katika barabara ya mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu.

Rais wa kitengo Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Mhadhiri wa majlisi hiyo alikuwa ni Shekhe Ali Shakuri, ameeleza historia ya mwenye tukio (a.s), qaswida na tenzi zikasomwa na Mula Ammaar Kinani, majlisi imehudhuriwa na viongozi wa mji wa Karbala pamoja na watumishi wa Ataba mbili tukufu”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na waombolezaji wa kifo cha Hamza bun Abdulmutwalib (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: