Majmaa-Ilmi inaendelea na semina ya tatu ya kuwajengea uwezo walimu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inaendelea na semina ya tatu ya kuwajengea uwezo walimu.

Kiongozi wa idara ya hauza katika Maahadi Shekhe Qudaamah Khadharami amesema “Semina hizi ni kwa ajili ya kukuza uwezo wa walimu katika kulea vipaji vya wanafunzi na kuwafanya kuwa msaada kwa jamii katika kutumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu”.

Akasema “Semina itadumu kwa muda wa siku nne mfululizo, wanafundishwa kwa ndadhariyya na vitendo, miongoni mwa masomo wanayofundishwa ni (Maarifa ya Qur’ani, Hukumu za usomaji, Kusimama na kuanza, Maandishi ya Qur’ani, Naghama, Misingi ya tafiti na njia za ufundishaji)”.

Washiriki wameridhishwa na semina hii, kutokana na faida kubwa inayopatikana ya kuinua viwango vyao vya elimu katika masomo ya Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: