Ofisi ya katibu mkuu inafanya semina ya ulinzi wa raia kwa watumishi wa Ataba tukufu.

Ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya semina ya ulinzi wa raia namba arubaini na tatu.

Semina hiyo imesimamiwa na idara ya usalama mahala pakazi na mbinu za kuzuwia matukio ya moto kwa kutumia vya zimamoto vya kushika mikononi.

Mkufunzi wa semina Ustadh Muhammad Kaamil Ni’mah amesema “Hii ni miongoni mwa semina zinazofanywa na idara ya usalama mahala pakazi kwa vitengo vya Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kujikinga na matukio ya moto”.

Akaongeza kuwa “Katika semina hiyo wamefundishwa aina za moto na uhakiki wa njia tatu pamoja na mbinu za kupambana na moto”.

Akaendelea kusema “Aidha wamefundishwa aina za zimamoto za kushika mkononi, mitambo ya kutoa tahadhari na mbinu za kudhibiti moto unaoanza kuwaka”.

Mwisho wa semina wamefanya mazowezi ya vitendo kwa yale waliyofundishwa na kuongeza mbinu mpya sambamba na uwezo wa watumishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: