Shirika la Alkafeel la uzalishaji limeanza kuvuna zaidi ya dunam 1200 za ngano.

Shirika la Alkafeel la uzalishaji katika Atabatu Abbasiyya limeanza kuvuna zaidi ya dunam 1200 za ngano kwenye mashamba yake.

Rais wa kitengo cha kilimo na ufugaji katika shirika hilo Mhandisi Ali Maz’al amesema “Shamba la ngano ni zaidi ya dunam 1200 pamoja na mazao mengine kama vile shairi, uvunaji huo unasimamiwa na watumishi wa kitengo chetu kutoka idara dofauti”.

Akaongeza kuwa “Shamba la ndano lipo katika mashamba ya Baraka za Ummul-Banina na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya shirika, tunatarajia mavuno ya msimu huu yakatuwa mazuri Insha-Alah”.

Akabainisha kuwa “Mazao yatapelekwa kwenye maghala ya wizara ya biashara, na sehemu nyingine yatatunzwa kwa ajili ya msimu ujao”.

Akasema kuwa “Shamba lina ngano za aina tofauti na zimelimwa na kutunzwa kwa njia tofauti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: