Kitengo cha habari na utamaduni kinafanya mihadhara ya kidini nchini Naijeria.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinafanya mihadhara ya Aqida na Fiqhi katika mji wa Kaduna nchini Naijeria.

Semina hiyo ni sehemu ya harakati za Markazi Dirasaati Afriqiyya kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika jamii za waafrika.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema: “Tunatuma mubalighina katika nchi za Afrika kufanya semina na kutoa mihadhara kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Mubalighi wa Markazi Shekhe Ibrahim Mussa ametoa mihadhara ya Aqida na Fiqhi katika mji wa Kaduna, amefafanua maswala ya kiitikadi na kifiqhi kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao katika bara la Afrika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: