Mhakiki Ashkuri amepongeza mafanikio ya kituo cha kitengo cha habari na utamaduni.

Allaamah Mhakiki Sayyid Ahmadi Husseini Ashkuri amepongeza mafanikio ya kituo cha kuhuisha turathi chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya.

Ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea kituo hicho na kukutana na kiongozi wa kituo Ustadh Muhammad Wakiil.

Mheshimiwa Wakiil ameeleza kwa ufupi miradi inayofanywa na kituo hicho, na miradi iliyokamilika.

Wamejadili mambo ya kielimu yanayo husu turathi pamoja na faida za turathi hizo.

Sayyid Ashkuri amefurahishwa kwa mafanikio aliyoyaona, aidha akapongeza harakati zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya, akawatakia mafanikio mema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: