Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani kwa jina la (Rahiqu-Tilawah) kwa ushiriki wa jopo wa wasomaji.
Vikao hivyo vinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya chini ya Majmaa.
Kikao cha kwanza kimefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na (Hussein Qazwini) halafu akafuatia (Hassan Janabi) kisha (Abdullahi Zuhairi Alhusseini) na mwisho msomaji wa Ataba mbili.
Inatarajiwa kufanyika vikao vya usomaji wa Qur’ani kila siku ya Ijumaa, kutakuwa pia na mihadhara ya kidini, utamaduni, mashindano ya kielimu pamoja na ratiba zingine za Qur’ani.