Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya nadwa kuhusu malengo ya kitivo cha udaktari.

Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya nadwa kuhusu malengo ya kitivo cha udaktari.

Watoa mada katika nadwa hiyo walikuwa ni rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali, mkuu wa kitivo Dokta Rahim Mahadi, baadhi ya watumishi, wahadhiri wa chuo na baadhi ya wanafunzi.

Katika nadwa hiyo wanafunzi wameonyesha baadhi ya harakati wanazofanya, sambamba na kueleza njia za ufundishaji na vituo vya tafiti za kielimu.

Baadhi ya tafiti zilizofanywa na wanafunzi zimejadiliwa katika nadwa hiyo, aidha umeongelewa ushirikiano baina ya chuo kikuu cha Al-Ameed na vyuo vingine kwa maslahi ya wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: