Atabatu Abbasiyya imekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran, yanayofanywa kwa mara ya thelathini na nne na yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho siku ya Alkhamisi.
Rais wa kamati ya maandalizi ya makongamano na mikutano ya kimataifa na rais wa kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Tumekamilisha maandalizi yote katika tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu kuelekea ushiriki wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa jijini Tehran, yanayo anza kesho siku ya Alkhamisi tarehe kumi na moja mwezi huu wa nne na yatadumu kwa muda wa siku kumi”.
Akaongeza kuwa “Tawi letu litaonyesha vitabu na machapisho yanayotolewa na Atabatu Abbasiyya, kikiwemo kitabu cha fatwa tukufu ya kujilinda ambacho kinashiriki kwa mara ya kwanza kwenye maonyesho hayo, pamoja na machapisho ya kituo cha kimataifa cha Al-Ameed, majarida na vitabu mbalimbali, aidha kutakuwa na kipengele cha barua kwa kaburi, ambapo watu wataandika barua na kupelekwa kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akabainisha kuwa “Tawi litakuwa na tv mbili kubwa zitakazo onyesha harakati mbalimbali zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.