Kitengo cha habari na utamaduni kimehudhuria kwenye kongamano la kielimu la kumi na tatu katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimehudhuria kongamano la kielimu la kumi na tatu kwenye chuo cha elimu za kisiasa Mustanswiriyya liitwalo (Mustaqbali wa idara, uhalisia na changamoto).

Kitengo cha hicho kimewakilishwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Kongamano hili linasaidia kujenga uzalendo na kufuata sheria katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi sambamba na kuishi kwa amani na watu tofauti katika jamii”.

Akaongeza kuwa “Markazi imeshiriki kwenye kongamano la kumi na tatu katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya, ikiwa ni sehemu ya ratiba endelevu ya kujenga ushirikiano na taasisi za kielimu hapa Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: