Rais wa kitengo Sayyid Riyaadh Hamza Ahmadi amesema “Leo tumetembelewa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini pamoja na wajumbe wa kamati kuu, wameangalia utendaji wetu wa kazi”.
Akaongeza kuwa “Mheshimiwa ameangalia utendaji kazi wa rasilimali watu kwa njia ya mtandao, kuanzia makazi, ruhusa, adhabu, mapumziko na mambo mengine yanayohusiana na watumishi wa Ataba tukufu”.
Akasisitiza kuwa “Mheshimiwa na wageni aliofuatana nao, wamepongeza utendaji wa kazi katika idara yetu na utaratibu unaotumika”.