Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil, imejadili njia za kushirikiana na kitivo cha elimu za kiislamu katika chuo kikuu cha Baabil.
Majadiliano hayo yamefanywa katika ziara iliyofanywa na ugeni wa Maahadi chini ya uongozi wa mkuu wa Maahadi hiyo, Sayyid Muntadhar Mashaikhi na viongozi wa idara ya elimu, baada ya kukutana na mkuu wa kitivo Dokta Hassan Ubaidi Maamuri na msaidizi wake Dokta Riyadhi Rahim Thu’bani.
Mashaikhi amepongeza kazi nzuri ya kuhamasisha usomaji wa Qur’ani katika mkoa wa Baabil inayofanywa na Maahadi sambamba na utayali wake wa kushirikiana na chuo kikuu cha Baabil kwa lengo la kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Katika ziara hiyo makubaliano yamefikiwa ya kufanya shughuli mbalimbali za Maahadi kwa kushirikiana na chuo kikuu katika mwaka wa masomo 2023/2024m.