Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya mahafali ya usomaji wa Qur’ani (Arshu-Tilawah) iliyohudhuriwa na wanafunzi wa Hauza.
Kiongozi wa idara ya harakati katika kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa Sayyid Wahaji Al-Abadi amesema “Mahafali hii ni muendelezo wa harakati ya (Arshu-Tilawah), imehudhuriwa kwa wingi na wanafunzi wa Hauza, ugeni wa wanafunzi wa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini unaofanya na Maahadi wa Qur’ani katika mji wa Najafu”.
Akaongeza kuwa “Miongoni mwa wahudhuriaji ni ugeni kutoka chama cha walezi wa watu wenye ulemavu, baadhi yao wameshiriki katika usomaji wa Qur’ani, sambamba na wasomaji wa Ataba tukufu na baadhi ya mashekhe”.
Mwanafunzi wa hauza Sayyid Abbasi Khaliil ameishukuru Atabatu Abbasiyya kwa kuwaalika wanafunzi wa Hauza, na kazi kubwa inayofanya ya kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu.