Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria amefanya kikao na idara ya wasimamizi wa haram na wahudumu wa mazuwaru.

Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Afdhalu Shami, amefanya kikao na watumishi wa idara ya wasimamizi wa haram tukufu, kuangalia huduma anazopewa mtu anayekuja kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria amesikiliza maelezo kutoka kwa watumishi na kupokea maoni yao, kuhusiana na utoaji wa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu na kuwawezesha kufanya ibada zao kwa amani na utulivu.

Mkuu wa idara Sayyid Aqiil Twaif amesema “Kikao kimelenga kuangalia changamoto wanazopata wahudumu na namna ya kuzitatua”.

Akaongeza kuwa “Maoni mbalimbali yanayo lenga kuboresha utendaji wa kazi za kila siku yametolewa kwenye kikao hicho”.

Kikao kimepambwa na majadiliano kuhusu namna bora ya kuhudumia mazuwaru wakati wa swala na njia nzuri za kuingia na kutoka ndani ya haram tukufu.

Sayyid Ahmadi Karim mmoja wa watumishi wa idara hiyo amesema “Tumemuambia Mheshimiwa kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria na mkuu wa idara ya usimamizi wa haram kuhusu uboreshaji wa huduma kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa “Tumesikiliza maoni muhimu yanayohusu uboreshaji wa huduma za kila siku kwa mazuwaru waliopo ndani ya haram tukufu”.

Naye Sayyid Haidari Rahim mmoja wa watumishi wa idara akasema, Hakika kikao hiki kimejadili njia bora za kuhudumia mazuwaru wakati wa swala na changamoto za uingiaji na utokaji ndani ya haram tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: