Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu wa sita Swadiq (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la watumishi wake.

Majlisi hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mhadhiri wa Majlisi Shekhe Naim Saaidi amesema “Majlisi ilikuwa na mada za aina tatu, kwanza historia ya Imamu wa sita, Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s) na namna alivyojitolea kwa ajili ya Dini tukufu ya kiislamu”.

Akaendelea kusema “Mada ya pili ilihusu elimu yake (a.s) katika fani za Fiqhi, Aqida, Historia na Kemiya”.

Amma mada ya tatu ilijikita katika vitendo na semi za Imamu Swadiq (a.s), kauli mbalimbali kutoka kwake zimetajwa sambamba na kuhimiza ufanyaji wa majlisi za kuomboleza misiba ya Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: