Mawakibu za Karbala zinaomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s).

Mawakibu za watu wa Karbala zimekuja kumpa pole bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kifo cha Imamu Swadiq (a.s).

Mawakibu za watu wa Karbala hufanya matembezi ya amani kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika kuomboleza matukio ya Ahlulbait (a.s).

Mula Salam Ibrahimi amesema “Kikundi cha vijana wa Ummul-Banina (a.s) na mawakibu za kuomboleza wamekuja kutoa pole kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s)” akabainisha kuwa “Mawakibu huja kutoa pole katika kila tukio la kifo cha Ahlulbait (a.s)”.

Kiongozi mmoja wa Mawakibu Sayyid Abduzahara Dabaghi amesema “Mawakibu za watu wa Karbala zimefanya matembezi kuanzia mlango wa Bagdad hadi haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: