Kitivo cha malezi katika chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata muhadhara kuhusu historia ya Imamu na dhulma alizofanyiwa katika Maisha yake sambamba na kueleza kazi kubwa ya kufundisha elimu aliyofanya na uchamungu wake.
Majlisi imefanywa saa tano ndani ya majengo ya chuo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.