Maahadi ya Qur’ani tawi la wasichana imepata muitikio mkubwa kwenye semina zake za majira ya kiangazi katika jiji la Bagdad.

Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imepata muitikio mkubwa kwenye semina za majira ya kiangazi, imepokea wanafunzi 100 kutoka shule za msingi.

Mkuu wa tawi la Maahadi katika jiji la Bagdad bibi Anwaru Abdurazaaq amesema “Tumepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi wa shule za msingi katika mji mkuu wa Bagdad”.

Akaongeza kuwa “Wanafunzi hao ni tabaka muhimu sana, wanatakiwa kutunzwa vizuri na kupewa elimu ya Qur’ani na maarifa ya haki”.

Akasema: “Wanafunzi wamewekwa kwenye madarasa Matano, wanafundishwa kwa utaratibu maalum, na bado idadi kubwa ya wanafunzi inaendelea kujitokeza”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: