Kitengo cha habari na utamaduni kinaandaa shindano la kielimu kwa wadau wa maonyesho ya vitavu ya kimataifa yatakayofanyika Najafu.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinaandaa shindano la kielimu kwa wadau wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa yatakayofanyika Najafu kwa awamu ya pili.

Kiongozi wa tawi Sayyid Muhammad A’raji amesema “Shindano litakuwa na maswali ya kielimu, kila mshiriki atachukua karatasi ya maswali na kuyajibu, washindi watapewa vitabu vilivyochapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa “Mashindano hayo yalipata mwitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru na waliomba yaandaliwe mashindano zaidi”.

Akafafanua kuwa “Lengo la kufanya mashindano haya ni kujenga uwelewa wa Dini na utamaduni katika jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: