Majmaa-Ilmi inawazawadia wanafunzi wa shule za sekula katika wilaya ya Hindiyya waliopata alama za juu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imewazawadia wanafunzi waliopata alama za juu katika wilaya ya Hindiyya, kama sehemu ya kuwatia moyo na kushajihisha wanafunzi wengine.

Hafla ya ugawaji wa zawadi imefanywa katika sekondari ya wavulana na kuhudhuriwa na viongozi wa shule na wazazi wa wanafunzi.

Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya Sayyid Haamid Mar’abi amesema “Mafanikio ya wanafunzi yametokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wazazi na walimu”.

Amehimiza wahudhuriaji wote waunge mkono harakati zinazofanywa na Maahadi ya Qur’ani zinazolenga kuhudumia vizito viwili vitakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: