Tambua kazi kubwa inayofanywa na idara ya usimamizi wa haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Idara ya usimamizi wa haram inaongoza matembezi ya kuingia na kutoka kwa mazuwaru ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara Sayyid Aqiil Twifu amesema “Wahudumu wa idara hii wanamajukumu mengi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni pamoja na kuongoza matembezi ya watu wanaoingia na kutoka ndani ya haram tukufu, kuweka misahafu, vitabu vya ziara na dua kwenye kabati za vitabu zilizopo ndani ya haram tukufu”.

Akaongeza kuwa “Miongoni mwa kazi zao pia ni kusafisha haram tukufu, miswala/ mazulia, feni, milango, taa, mapambo yaliyopo kwenye kuta na dari, kupuliza marashi sambaba na kusaidia kubeba wazee wasiojiweza na watu wenye ulimavu kwa kutumia viti-mwendo”.

Akasema kuwa “Wahudumu wa idara yetu wanatoa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru, hufanya kila wawezalo kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru ndani ya Ataba tukufu, ili kurahisisha shughuli zao na kuhakikisha wanafanya ibada kwa amani na utulivu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: