Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imepata muitikio mkubwa wa wanafunzi watakaoshiriki kwenye semina za kiangazi katika wilaya ya Hindiyya.
Mkuu wa Maahadi bibi Nida Abdusajaad amesema “Maahadi imepokea zaidi ya wanafunzi (350) katika ofisi ya tawi na vituo vilivyo chini yake, kwa lengo la kuwafundisha mabinti hao mambo yenye faida kwao duniani na akhera”.
Akaongeza kuwa “Wanafunzi (172) wameandikishwa kwenye kituo cha nje chini ya tawi la Maahadi ya Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya”.
Maahadi inaendelea kupokea wanafunzi watakaoshiriki kwenye semina za kiangazi.