Majmaa-Ilmi imeanza mradi wa kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani katika mkoa wa Karbala.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeanza mradi wa kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani tukufu.

Mradi huo unasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Kiongozi wa idara ya tahfidh katika Maahadi Shekhe Ali Rawii amesema “Kupitia mradi wa kujengea uwezo wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani katika mkoa wa Karbala, tumepokea wanafunzi (20) waliohifadhi juzuu tofauti za Qur’ani, mradi huu utadumu kwa muda wa siku (60) kila siku watasoma kurasa (50) za Qur’ani sambamba na kutwalii sehemu waliyo hifadhi”.

Akafafanua kuwa: “Mradi unafanywa katika nyakati mbili, asubuhi na jioni, Maahadi imeandaa sehemu nzuri za kusomea, vipaza sauti, kumbi za kutolea mihadhara, vyumba vya kupumzika, chakula na sehemu ya michezo kwa ajili ya kupumzisha akili zao”.

Akasema kuwa, lengo la mradi huu ni kujenga uwezo wa kuhifadhi Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: