Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amehusia watumishi wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu kutumia likizo za kiangazi kufanya program za Qur’ani.
Ameyasema hayo kwenye mkutano uliofanywa leo ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu.
Akasema kuwa “Miongoni mwa shughuli za Ataba tukufu ni harakati za Qur’ani, katika msimu wa masomo au likizo, lengo kubwa huwa ni kutumia kila fursa, sambamba na kulenga wanufaika wa umri tofauti”.
Akaongeza kuwa “Qur’ani tukufu ni kitu muhimu kwa mwanaadamu, anatakiwa atafakari aya zake na kunufaika nazo kwa kufata maelekezo yake katika maisha ya kila siku, bila shaka vipaombele vya wanaadamu vinatofautiana, kunawanaojali mali, umashuhuri, starehe za dunia na kuna wanaojali Qur’ani tukufu, wanazipamba sauti zao kwa kusoma Qur’ani kwa namna ambayo mtu anapenda kusikiliza”.
Akaendelea kusema “Wanafunzi wanaelekea kwenye likizo za kiangazi na wanatakiwa wanufaike na kipindi cha likizo kwa kupewa muongozo wa mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na Qur’ani tukufu”.