Kitengo cha Maqaam kinasafisha ukumbi wa haram na kutandika mazulia.

Kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) katika Atabatu Abbasiyya, kinasafisha ukumbi wa haram na kutandika mazulia.

Rais wa kitengo Sayyid Adnani Dhaifu amesema “Watumishi wa kitengo chetu wametandika mazulia mapya ndani ya ukumi wa Maqaam tukufu”.

Akaendelea kusema “Pamoja na kazi ya kutandika mazulia, wamesafisha kila sehemu ya Maqaam takatifu”, akabainisha kuwa “Kazi hizi hufanywa kila wakati chini ya utaratibu maalum”.

Kitengo kimeweka mazingira mazuri kwa mazuwaru watukufu wanaokuja kutembelea Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) na kuhakikisha wanafanya ibada kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: