Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Ridhwa na dada yake Sayyidah Maasumah (a.s).

Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Ridhwa na dada yake bibi Fatuma Maasumah (a.s).

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, baada ya Qur’ani mshairi Zainul-Aabidina Saidi na Muhammad Faatwimi wakapanda kwenye mimbari kisha waimabi mahiri wa qaswida Sayyid Hamudi Mussawi, Sayyid Ibrahimu Sharifi na Sayyid Ali Ambari nao wakapanda kwenye mimbari.

Rais wa kitengo cha Habari na utamaduni katika Ataba tukufu Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Atabatu Abbasiyya inatilia umuhimu kuhuisha matukio ya Maimamu wa Ahlulbaid (a.s), sambamba na kuadhimisha mazazi ya Imamu Ridhwa na dada yake bibi Fatuma Maasumah (a.s), hafla hii imefanywa kwa ajili ya watukufu hao wawili (a.s)”.

Akabainisha kuwa “Hafla imeshuhudia muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), imeandaliwa sehemu maalum katika barabara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya mlango wa Qibla kwa ajili ya kufanya hafla hiyo, mawakibu, vikundi vya Husseiniyya na wakazi wa mji wa Karbala wameshiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: