Majmaa-Ilmi imetangaza kuanza kusajili washiriki wa semina za majira ya kiangazi katika mji wa Karbala.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imetangaza kuanza kwa usajili wa washiriki wa semina za majira ya kiangazi katika mji wa Karbala.

Semina zinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Karbala chini ya Majmaa.

Usajili utaanza rasmi siku ya Jumanne ya tarehe 23/05/2023 hadi jioni ya Jumapili ya tarehe 28/05/2023, kwa kila anayetaka kujisajili afike kwenye vituo vya usajili vilivyopo:

  • 1- Shule za Al-Ameed za wavulana karibu na malalo ya Huru (a.s) kuanzia saa 4 Asubuhi hadi saa 11 Alasiri, usajili huo unahusisha mitaa yote ya mkoa wa Karbala ispokua (kituo cha mji mkongwe).
  • 2- Haram ya Abbasi (Sardabu ya Imamu Hassan -a.s-) kuanzia saa 2 Asubuhi hadi saa 6 Adhuhuri. Kumbuka kuwa usajili unawahusu wakazi wa eneo la ujini peke yake na hakuna sharti la huduma ya usafiri.

Usajili unawahusu vijana wa kiume peke yake, inahitajika idadi maalum, wakati wowote idadi ikitimia usajili utasimamishwa, kila muombaji anatakiwa kuleta picha mbili ndogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: