Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza nafasi za kazi kwa wahitimu wa shahada ya udaktari katika fani zifuatazo:
Dokta wa Biochemistry.
Dokta wa Biology.
Dokta wa Tissue.
Dokta wa Physics.
Dokta wa Organic Chemistry.
Dokta wa Microscopy.
Mtu yeyote mwenye elimu tajwa hapo juu na anayependa kufanya kazi kwetu, atume maombi akiambatanisha na wasifu (cv) katika ofisi ya makamo rais wa chuo, maombi yanapokelewa kuanzia siku ya Jumatatu (22/5/2023) hadi siku ya Alkhamisi mwezi huu.
Tambua kuwa ofisi za chuo zipo barabara ya (Karbala – Najafu) mkabala na nguzo namba 1238.