Waziri wa utamaduni amesema: Makubaliano yetu ya Atabatu Abbasiyya yanalenga kuhifadhi nakala-kale na kuzifikisha kwa watafiti.

Waziri wa utamaduni na utalii Dokta Ahmadi Badrani amesema kuwa ushirikiano kati ya Atabatu Abbasiyya na wizara unalenga kuhifadhi nakala-kale na kuzifikisha kwa watafiti.

Akaongeza kuwa “Makubaliano yanahusu uhakiki na utunzaji wa nakala-kale chini ya wizara, sambamba na uwezekano wa kubadilishana uzowefu na kuweka taarifa kwenye mtandao kwa lengo la kuzifikisha kwa watafiti”.

Badrani amepongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutunza hazina hiyo pamoja na changamoto kubwa iliyolikuta taifa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: