Kitengo cha habari kimechapisha toleo jipya la jarida lakitafiti.

Hivi karibuni kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kupitia kituo cha kiislamu na masomo ya kimkakati kimechapisha toleo la thelathini na nne la jarida.

Toleo jipya limeandika maudhui zinazohusu turathi, miongoni mwake ni (Istishraaq za aina tofauti kwa lengo moja, kujenga mtazamo wa mustashriqina mbele ya ubora wa Qur’ani, mfumo wa Filoloji mbele ya Mustashriqina).

Miongoni mwa mambo yaliyomo pia ni (Mustashriqina katika ngome ya Qur’ani, fikra za Mustashriq katika maandishi ya wanahistoria, nafasi ya masomo ya Istishraqiyyah katika masomo ya athari za tamaduni, uhai wa Muhammad au wakati wa kuonyesha uhakika kamili).

Jarida linalenga kupunguza uhaba wa majarida ya kielimu na kitafiti katika maktaba za kiislamu sambamba na kwenye mfumo wa masomo ya kisekula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: