Atabatu Abbasiyya yakamilisha wajibu wake katika maeneo manne kwenye mradi wa mkanda wa kijani.

Atabatu Abbasiyya imeandaa maeneo manne ya mkanda wa kijani, katika mradi wa mkanda wa kijani wa kusini wenye maeneo 22.

Kiongozi wa mkanda wa kijani wa kusini Sayyid Naasir Husseini Mut’ibu amesema: “Tumeanza kuandaa zaidi ya maeneo 22, maeneo manne yamefungua milango mbele ya wakazi, kila eneo linaukubwa wa dunam 25 na limekutana na chanzo cha maji na umeme upo”.

Akaongeza kuwa “Kila eneo linasehemu kubwa ya kijani, linataa na mitambo ya umwagiliaji, sehemu za kupumzika familia sambamba na sehemu za ndege na wanyama”

Akabainisha kuwa “Kazi hiyo imefanywa baada ya Ataba kuchukua jukumu la kupanda miti kwa lengo la kuandaa sehemu ya kupumzikia familia za watu wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: