Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imefungua kituo cha ushonaji wa sare za wanafunzi.

Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefungua kituo cha ushonaji wa sare za wanafunzi wa masomo ya Qur’ani.

Kiongozi wa kituo hicho bibi Zainabu Aljaburi amesema “Ufunguzi wa kituo hiki ni sehemu ya maandalizi maalum ya hafla ya kuwajibikiwa na sheria wanafunzi wa kozi za Qur’ani kwa mwaka wa pili mfululizo, imechaguliwa sare nyeupe kama ishara nafsi safi na roho nzuri”.

Akaongeza kuwa “Walimu walianza kazi miezi mitatu iliyopita na kazi bado inaendelea ya kushona sare 250 za wanafunzi wa Maahadi ya Najafu na matawi yake ya mikoani”.

Maahadi inafundisha Qur’ani chini ya mwamvuli wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa mujibu wa maelezo ya Ajaburi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: