Rais wa kitengo cha habari na utamaduni amekutana na mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya.

Rais wa kitengo cha Habari na utamaduni Sayyid Aqiil Yaasiri amekutana na mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Shimri, kwa ajili ya kufuatilia maandalizi ya kongamano la wiki ya Uimamu ya kimataifa.

Katika mkutano huo wameangalia mada zitakazo wasilishwa kwenye kongamano hilo litakalo simamiwa na Ataba tukufu na kuangalia ratiba na harakati za Markazi na idara zake sambamba na mkakati wa kitablighi.

Shimri akasisitiza kuwa “Markazi inatumia uwezo wake wote kwa ajili ya kufanikisha kongamano hilo, hakika Markazi inamchango mkubwa katika hili”.

Akabainisha kuwa “Markazi inaendelea kufanya program na harakati mbalimbali za kitablighi, kielimu na kibinaadamu katika bara la Afrika pamoja na kusaidia familia za waafrika wanaoishi Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: