Sayyid Swafi amefanya mazungumzo na Sayyid Ashkuri kuhusu uboreshaji wa sekta ya turathi.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amefanya mazungumzo na mhakiki Sayyid Ahmadi Ashkuri kuhusu uboreshaji wa sekta ya turathi.

Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Mheshimiwa Sayyid Ashkuri kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu.

Rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Ammaar Hilali amesema “Sayyid Ahmadi Ashkuri katika mazungumzo yake na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmazi Swafi, ameeleza njia za uboreshaji wa sekta ya turathi chini ya Ataba, taasisi na vituo vya turathi vinavyo milikiwa na Ataba”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya ni kinara katika sekta ya turathi, inataasisi na vituo vingi vya faharasi na uhakiki wa turathi, aidha imeshapata tuzo nyingi za kimataifa katika sekta hiyo na imechapisha vitabu vya uhakiki wa faharasi na turathi”.

Shekhe Hilali akabainisha kuwa “Kikao kilikuwa na faida kubwa, mapendekezo mbalimbali yametolewa kuhusu namna ya kuboresha sekta hiyo chini ya taasisi zinazomilikiwa na Ataba pamoja na uzowefu wake katika sekta hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: