Ugeni wa Majmaa-Ilmi umefanya warsha ya kuwajengea uwezo walimu wa semina za majira ya kiangazi katika mji wa Baabil.

Ugeni wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, umefanya warsha ya kuwajengea uwezo walimu wa semina za Qur’ani zitakazofanywa msimu wa joto katika kitongoji cha Abu Gharq na Hamza magharibi ya mji wa Baabil.

Semina hizo zitasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa, warsha hiyo ni sehemu ya maandalizi ya semina za Qur’ani kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Ugeni umesisitiza kuwa, mambo muhimu yatakayofundishwa kwenye semina hizo ni njia za ufundishaji zitakazotumika kwenye somo la Qur’ani na Aqida.

Semina hizo zitafanywa kwenye vitongoji vyote vya Baabil, kwa lengo la kuongeza uwezo wa walimu wa mradi wa Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: