Kitengo cha mahusiano kimeandaa na kusimamia ziara ya kwenda Najafu kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya.

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa na kusimamia ziara ya kwenda Najafu kwa watumishi wa Ataba.

Kiongozi wa idara ya mahusiano ya ndani Sayyid Rasuul Naaji amesema kuwa “Kitengo kimeandaa ziara ya kwenda Najafu kutembelea malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) na Maraajii watukufu kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya”.

Akaongeza kuwa “Idara ya kupokea wageni wa Maraajii, imepokea watumishi wa Atabatu Abbasiyya 75 katika ratiba hiyo”.

Ratiba imedumu kwa muda wa siku tato, mambo tofauti yamefanywa, ikiwa ni pamoja na utowaji wa mihadhara mbalimbali, mashindano na kutembelea maeneo tofauti ya kihistoria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: