Msimamizi wa Maqaam ya Samaraa Sayyid Bakri Muhammad Sharifu amesifu kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya ujenzi na uhandisi wa majengo.
Akasema: “Tumekuja kufanya ziara katika Ataba tukufu na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, tumesha kubaliana mfumo tutakaotumia wakati wa ziara ya Arubaini, ili kuwafanya mazuwaru wajue umuhimu wa Samaraa na tutaendelea kushirikiana katika kufanikisha hilo”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya majengo na ufanisi wa kihandisi na imepata mafanikio katika jambo hilo”.
Akamaliza kwa kushukuru Ataba kwa namna inavyo jitolea katika kuhudumia jamii na mazuwaru.