Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetaja mkakati wake katika kuhudumia mazuwaru wakati wa msimu wa kiangazi kipindi cha joto kali.
Makamo rais wa kitengo hicho Mhandisi Abbasi Ali amesema “Kitengo kimefanya maandalizi kadhaa kufuatia kuingia kwa msimu wa joto, tumeweka hodhi za maji (150) ndani ya haram tukufu ya Abbasi sambamba na kuweka deli (150) upande wa mlango wa Kibla na kwenye barabara zinazo elekea Ataba”.
Akaongeza kuwa “Madeli yanawekwa maji na barafu wakati wote, ili kuhakikisha mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanapata maji safi na baridi ya kunywa”.
Akafafanua kuwa “Madeli ya maji yanawekwa vipande (150) vya barafu kila siku, sambamba na kuwekewa miamvuli kwa ajili ya kuyakinga na mionzi ya jua na kufanya ubaridi udumu kwa muda mrefu”.