Kitengo cha habari kitafanya muhadhara kuhusu ukafiri wa sasa.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa semina kuhusu nafasi ya (ukafiri wa sasa).

Semina itasimamiwa na kituo cha kiislamu na tafiti za kimkakati ikiwa ni sehemu za mkakati wa Ataba katika sekta ya Dini na kupambana na fikra potofu.

Semina itafanywa kupitia mtandao wa zoom kuanzia saa kumi na moja Alasiri siku ya Jumapili ya tarehe (28/5/2023m) hadi tarehe (1/6/2023m) chini ya uhadhiri wa Shekhe Ali Dilani.

Semina hii ni sehemu ya harakati za kituo cha kiislamu katika kulinda na kuhifadhi misingi ya elimu na itikadi ya dini tukufu ya uislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: