Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kitatoa mihadhara kwa njia ya mtandao inayowalenga wanawake, yenye anuani isemayo (Tofauti ya akili ya mwanamke na mwanaume).
Maswali tofauti yataulizwa na kujadiliwa, miongoni mwa maswali hayo ni: Je kunatofauti kati ya akili ya mwanamke na mwanaume? Kwa nini baadhi ya wanaume hujitoa linapotokea tatizo fulani? Ni vipi vipaombele vya mwanaume na ni vipi vya mwanamke? Upi ushirikiano bora katika Maisha ya ndoa.
Muhadhara utatolewa tarehe (3/6/2023m) saa tano asubuhi kupitia jukwaa la telegram kwa link ifuatayo: https://t.me/alecture1