Chuo kikuu cha Al-Ameed kupitia rais wa chuo hicho Dokta Muayyad Imrani Alghazali kimefanya kikao na kamati ya wahariri wa jarida la chuo kikuu cha Al-Ameed la tafiti za kielimu, kama sehemu ya kujiandaa kutoa chapisho la kwanza la jarida hilo.
Mkutano huo wamejadili hatua waliyopo katika uandaaji wa jarida hilo, kiongozi wa kamati ya wahariri Dokta Hussein Alawi Alghanimi ametoa maelezo ya kina kuhusu uandaaji wa jarida hilo na namna wanavyo shirikiana na (Editorial manager) kupitia uratibu wa idara ya jarida (relatedinner).
Kikao hicho kimeshuhudia mambo muhimu ya tafiti za kielimu yaliyo andikwa kwenye jarida hilo na yaliyo kataliwa na wachambuzi wa kielimu.