Wamekutana katika ukumbi wa utawala ndani ya Ataba tukufu, kwa kushirikiana na kitengo cha Maadhimisho na Mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Kiongozi wa Maukibu ya Baabu-Khani Shekhe Abdu-Ali Alhamiri amesema “Leo tumekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Aalu Dhiyaau-Dini na kujadili changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na muda ambao hupewa mawakibu Husseiniyya katika mwezi wa Muharam”.
Akaongeza kuwa “Kila mwaka kabla ya kuingia mwezi mtukufu wa Muharam huwa tunakaa na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Mawakibu Husseiniyya pamoja na kuandaa ratiba ili kuondoa mgongano baina yetu, na kuhakikisha matembezi ya mawakibu yanafanyika vizuri kuanzia eneo la Mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na ndani ya haram zenyewe takatifu”.