Idara inayosimamia haram tukufu chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya inasimamia matembezi ya mazuwaru ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuweka mazingira mazuri kiroho.
Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Aqiil Qassim Twaif amesema kuwa, wahudumu wa idara wanajitahidi kuweka mazingira mazuri kiroho ndani ya haram tukufu na kurahisisha ibada ya ziara mbele ya kaburi tukufu.
Akaongeza kuwa, wahudumu wetu wanafanya usafi wakati wote kwa utaratibu maalum.
Miongoni mwa majukumu yetu pia ni kusafisha Maqaam ya Imamu wa zama (a.f), kupamba kaburi katika tarehe za kumbukumbu za mazazi na kuweka vitambaa vyeusi katika kumbukumbu za vifo.