Wizara ya elimu ya juu imesema: Chuo kikuu cha Alkafeel kimekamilisha vigezo vya kuanzisha kituo cha elimu endelevu.

Mkuu wa kitengo cha elimu katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu Dokta Haidari Swabahi amesema kuwa, chuo kikuu cha Alkafeel kimekamilisha vigezo vya kiidara na kimazingira vya kuanzisha kituo cha elimu endelevu.

Ameyasema hayo baada ya kamati yake kutembelea chuo hicho na kuangalia maandalizi ya kuanzishwa kituo cha elimu endelevu.

Kamati hiyo imegagua majengo, kumbi za madarasa na vitengo vya kielimu, wakiwa pamoja na rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani na Dokta Nawaal Aaid Almayali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: